Nina haja nawe, kila saa;
Hawezi mwingine, kunifaa.

Yesu, nakuhitaji,
Vivyo kila saa!
Niwezeshe, Mwokozi,
Nakujia.

Nina haja nawe; Kaa nami,
Na maonjo haya, Hayaumi.

Yesu, nakuhitaji,
Vivyo kila saa!
Niwezeshe, Mwokozi,
Nakujia.

Nina haja nawe; Kila hali,
Maisha ni bure, uli mbali.

Yesu, nakuhitaji,
Vivyo kila saa!
Niwezeshe, Mwokozi,
Nakujia.

Nina haja nawe; nifundishe,
Na ahadi zako, zifikishe.

Yesu, nakuhitaji,
Vivyo kila saa!
Niwezeshe, Mwokozi,
Nakujia.

Nina haja nawe;  Mweza yote;
Ni wako kabisa, Siku zote.

Yesu, nakuhitaji,
Vivyo kila saa!
Niwezeshe, Mwokozi,
Nakujia.