Kaa nami, ni usiku tena;
Usiniache gizani Bwana;
Msaada wako haukomi;
Nilipeke yangu kaa nami.
Siku zetu hazikawi kwisha;
Sina mwingine wa kunifaa;
Mimi nitaongozwa na nani;
Ila wewe Bwana, kaa nami.
Sichi neno uwapo karibu;
Nipatalo lote si taabu;
Kifo na kaburi haviumi;
Nitashinda kwako, kaa nami.
Nilalapo nikuone wewe;
Hata gizani nimulikiwe;
Nuru za mbinguni hazikomi;
Siku zangu zote, kaa nami.