Baraka zake ni nyingi, 
asema Bwana Mungu,
Siku zake za furaha, 
zakaribia kwetu.

Utubariki, 
Roho Mtakatifu,
Tusipokee kiasi, 
bali tujazwe kweli.

Baraka zake ni nyingi, 
zafurahisha myoyo,
Mungu azitume kwetu, 
Baraka ndiye Roho.

Utubariki, 
Roho Mtakatifu,
usipokee kiasi, 
bali tujazwe kweli.

Baraka zake ni nyingi, 
ndizo tunangojea,
Mpaka litangazwe pote 
Neno la Mungu wetu.

Utubariki, 
Roho Mtakatifu,
Tusipokee kiasi, 
bali tujazwe kweli.

Baraka zake ni nyingi, 
utume kwetu leo,
Tungali tunakuomba, 
utubariki Bwana.

Utubariki, 
Roho Mtakatifu,
Tusipokee kiasi, 
bali tujazwe kweli.