Popote na Yesu nina amani,
Pote
aniongozapo nchini,
Asipokuwapo sina furaha,
Popote
na Yesu sitaogopa.
Popote, popote, sitaogopa,
Popote na Yesu mimi salama.
Sina upungufu awapo Yesu,
Hatajaribuni niingiapo,
Alijaribiwa anishindie,
Popote na
Yesu mimi mshindaji.
Popote, popote, sitaogopa,
Popote na Yesu mimi salama.
Popote na Yesu hataniacha,
Ingawa
wataniacha wengine,
Hata aniongoze taabuni,
Popote na
Yesu nitashukuru.
Popote, popote, sitaogopa,
Popote na Yesu mimi salama.
Pote duniani na baharini,
Niwatangazie wote wokovu,
Ni tayari kwenda aniitapo,
Njia
zote upendoni mwa Yesu.
Popote, popote, sitaogopa,
Popote na Yesu mimi salama.
Popote na Yesu si hatarini,
Nijapozungukwa sana na giza,
Nitaamka salama mbinguni,
Kukaa
pamoja naye milele
Popote, popote, sitaogopa,
Popote na Yesu mimi salama.