Umechoka hata kuzimia?
Mwambie Yesu, Mwambie Yesu,
Je, huna furaha na amani?
Mwambie Yesu pekee.
Mwambie Yesu, mwambie Yesu,
Msaidizi kweli,
Hutapata mwingine kama Yeye,
Mwambie Yesu pekee.
Mbona una huzuni rohoni?
Mwambie Yesu, Mwambie Yesu,
Dhambi zako mbona zakushinda?
Mwambie Yesu pekee.
Mwambie Yesu, mwambie Yesu,
Msaidizi kweli,
Hutapata mwingine kama Yeye,
Mwambie Yesu pekee.
Watu wengi wanakuchukia?
Mwambie Yesu, Mwambie Yesu,
Shaka unayo juu ya kesho,
Mwambie Yesu pekee.
Mwambie Yesu, mwambie Yesu,
Msaidizi kweli,
Hutapata mwingine kama Yeye,
Mwambie Yesu pekee.
Waogopa kifo na mauti?
Mwambie Yesu, Mwambie Yesu,
Omba Yesu arudi upesi,
Mwambie Yesu pekee.
Mwambie Yesu, mwambie Yesu,
Msaidizi kweli,
Hutapata mwingine kama Yeye,
Mwambie Yesu pekee.