Yesu kwetu ni rafiki,
Haja zote hujua,
Tukiomba kwa Babaye
Maombi  asikia,
Lakini twajikosesha,
Twajitweka vibaya,
Kwamba tukimwomba Mungu,
Dua atasikia.

Una dhiki na maonjo?
Una mashaka pia?
Haifai kufa moyo,
Dua atasikia.
Hakuna mwingine mwema
Wa kutuhurumia
Atujua tu dhaifu,
Maombi asikia.

Je, hunazo hata nguvu,
Huwezi  kwendelea?
Ujapodharauliwa,
Ujaporushwa pia,
Watu wangekudharau,
Wapendao dunia
Hukwambata mikononi,
Dua atasikia.