Namwandama Bwana kwa alilonena,
Njia yangu huning'azia;
Nikimridhisha atanidumisha
Taamini nitii pia.

Amini utii, njia pweke ni hii
Ya furaha kwa yesu, amini ukatii



Giza sina kwangu wala hata wingu
Yeye mara huviondoa
Woga wasiwasi, sononeko basi.
Huamini nitii pia.

Amini utii, njia pweke ni hii
Ya furaha kwa yesu, amini ukatii

Masumbuko yote, sikitiko lote;
Kwa mapenzi hunilipia,
Baa, dhara, dhiki, vivyo hubariki,
Taamini nitii pia.

Amini utii, njia pweke ni hii
Ya furaha kwa yesu, amini ukatii

Mimi sitajua raha sawasawa
Ila yote yesu kumpa;
Napata fadhili na radhi kamili,
Taamini nitii pia.

Amini utii, njia pweke ni hii
Ya furaha kwa yesu, amini ukatii

Nitamfurahisha na kumtumaini,
Majumbani na njia-njia;
Agizo natenda; nikitumwa hwenda,
Huamini nitii pia

Amini utii, njia pweke ni hii
Ya furaha kwa yesu, amini ukatii