Mteteeni Yesu,
Mlio Askari;
Inueni Beramu,
Mkae Tayari;
Kwenda Naye Vitani
Sisi Hatuchoki
Hata Washindwe Pia
Yeye Amiliki.

Mteteeni Yesu,
Vita Ni Vikali;
Leo Siku Ya Bwana,
Atashinda Kweli;
Waume Twende Naye,
Adui Ni Wengi,
Lakini Kwake Bwana
Tuna Nguvu Nyingi.


Mteteeni Yesu,
Wenye Ushujaa
Nguvu Zenu Za Mwili
Hazitatufaa;
Silaha Ya Injili
Vaeni Daima;
Kesheni Mkiomba;
Sirudini Nyuma.    

Mteteeni Yesu,
Vita Ni Vikali,
Wengi Wamdharau,
Hawamkubali;
Ila Atamiliki
Tusitie Shaka;
Kuwa Naye Vitani

Twashinda Hakika.

Play the YouTube video below, turn up the speakers, and sing along in Swahili!