Mungu mtukufu aliye Bwana
Akamtoa Yesu mwana mpendwa
Akawa dhabihu kwa dhambi zote
Kufungua njia kwa watu wote
Msifuni, msifuni Nchi imsikie
Msifuni, msifuni, Bwana mshangilie
Njoni kwake Baba, kwa Yesu Mwana
Mpeni heshima, aliye Bwana
Ukombozi wetu, tendo la Mungu
Ni ukamilifu kwa kila mtu
Mwenye ukosefu akimwamini
Atasamehewa na Yesu, kweli
Msifuni, msifuni Nchi imsikie
Msifuni, msifuni, Bwana mshangilie
Njoni kwake Baba, kwa Yesu Mwana
Mpeni heshima, aliye Bwana
Ametufundisha mambo ya mbingu
Tukafurahishwa na Mwana Mungu
Ametuinua tukae naye
Atatuongoza hata milele
Msifuni, msifuni Nchi imsikie
Msifuni, msifuni, Bwana mshangilie
Njoni kwake Baba, kwa Yesu Mwana
Mpeni heshima, aliye Bwana