Bwana hunificha mafichoni mwake,
Hunifariji matesoni mwote,
Nimepata mapumziko kwake Yesu,
Hunilinda njiani pote.

Hunificha mafichoni,
Nionapo majaribu na mateso,
Hunificha mafichoni,
Bwana hunificha mafichoni mwake.

Bwana hunificha mafichoni mwake,
Ninalindwa naye utukufuni,
Nimevikwa na mwangaza wa mwokozi,
Ninafurahi siku zote.

Hunificha mafichoni,
Nionapo majaribu na mateso,
Hunificha mafichoni,
Bwana hunificha mafichoni mwake.

Bwana hunificha mafichoni mwake,
Mafichoni mwake hubarikiwa,
Nimefunguliwa na Mkombozi wangu,
Nani atakayenishinda?

Hunificha mafichoni,
Nionapo majaribu na mateso,
Hunificha mafichoni,

Bwana hunificha mafichoni mwake.